Isaiah 46:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe Beli umeanguka; Nebo umeporomoka. Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu. Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama, hao wanyama wachovu wamelemewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Beli anasujudu, Nebo anainama; sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo. Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, mzigo kwa waliochoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Beli anaanguka chini, Nebo anainama; sanamu zao ziko juu ya wanyama, na juu ya ng'ombe; vitu vile mlivyokuwa mkivichukua huku na huku vimekuwa mzigo, mzigo wa kumlemea mnyama aliyechoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe Beli umeanguka; Nebo umeporomoka. Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu. Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama, hao wanyama wachovu wamelemewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama; sanamu zao hubebwa na wanyama wa mizigo. Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, mzigo kwa waliochoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama; sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo. Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, mzigo kwa waliochoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Beli anaanguka chini, Nebo anainama; sanamu zao ziko juu ya wanyama, na juu ya ng'ombe; vitu vile mlivyokuwa mkivichukua huku na huku vimekuwa mzigo, mzigo wa kumlemea mnyama aliyechoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe Beli umeanguka; Nebo umeporomoka. Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu. Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama, hao wanyama wachovu wamelemewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Beli ameanguka, Nebo naye yuko chini, vinyago vyao viko migongoni kwa punda na ng'ombe; vilivyotembezwa nanyi vimefungwa, ikawa mizigo ya kuchokesha nyama wanaoichukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Beli anaanguka chini, Nebo anainama; sanamu zao ziko juu ya wanyama, na juu ya ng’ombe; vitu vile mlivyokuwa mkivichukua huku na huku vimekuwa mzigo, mzigo wa kumlemea mnyama aliyechoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ule mungu Bali ameanguka; mungu Nebo anainama. Sanamu zao zinabebwa juu ya nyama, juu ya nyama wanaobeba mizigo! Vitu ninyi mulivyokuwa mukiviinua juu, vinakuwa sasa mizigo, vinakuwa mizigo mizito juu ya nyama wenye kuchoka.