Isaiah 46:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo, nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli. Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa; niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo, ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba, nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo, nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli. Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa; niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nisikilizeni mimi, Ee nyumba ya Yakobo, ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba, nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo, ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba, nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo, nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli. Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa; niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nisikilizeni, ninyi mlio wa mlango wa Yakobo! Ninyi wote mlio masao ya mlango wa Isiraeli! Ninyi ndio, niliojitwika tangu hapo, mlipokuwa tumboni mwa mama zenu, ninyi ndio, niliojichukuza tangu hapo, mlipozaliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize, enyi wazao wa Yakobo, munisikilize, enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli. Mimi niliwatunza ninyi tangu mulipozaliwa; niliwabeba ninyi tangu katika tumbo la mama yenu.