Isaiah 46:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba, kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo; kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo. Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia, wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huiinua mabegani na kuichukua; huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo. Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale. Ingawa mtu huililia, haimjibu; haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa na taabu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba, kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo; kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo. Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia, wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huiinua kuiweka mabegani na kuichukua; huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo, wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale. Ingawa mtu huililia, haijibu; haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huiinua mabegani na kuichukua; huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo. Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale. Ingawa mtu huililia, haimjibu; haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa kutoka kwa taabu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba, kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo; kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo. Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia, wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha huuchukua mabegani, huutembeza, kisha huuweka mahali pake; hapo unasimama pasipo kuondoka mahali pake. Wanapoulilia, hauwaitikii; hakuna, umwokoaye katika shida yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa na taabu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanajibebesha sanamu hiyo juu ya mabega na kuipeleka, kisha wanaiweka pahali pake, nayo inakaa palepale; haiwezi hata kidogo kusogea kutoka pale inapokuwa. Mutu akiililia, haiwezi kumwitikia, wala haiwezi kumwokoa mutu katika taabu zake.