Isaiah 47:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini maafa yatakupata ambayo hutaweza kujiepusha nayo. Balaa litakukumba ambalo hutaweza kulipinga; maangamizi yatakujia ghafla ambayo hujapata kamwe kuyaona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafa yatakujia, nawe hutaweza kuyaondoa kwa uaguzi. Janga litakuangukia, wala hutaweza kulikinga kwa fidia; msiba mkuu usioweza kuutabiri utakujia ghafula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini maafa yatakupata ambayo hutaweza kujiepusha nayo. Balaa litakukumba ambalo hutaweza kulipinga; maangamizi yatakujia ghafla ambayo hujapata kamwe kuyaona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafa yatakujia, nawe hutaweza kuyaondoa kwa uaguzi. Janga litakuangukia wala hutaweza kulikinga kwa fidia; msiba mkuu usioweza kuutabiri utakujia ghafula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafa yatakujia, nawe hutaweza kuyaondoa kwa uaguzi. Janga litakuangukia, wala hutaweza kulikinga kwa fidia; msiba mkuu usioweza kuutabiri utakujia ghafula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo uovu utakupata; wala hutaweza kuuagua; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa usioujua utakupata kwa ghafla.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini maafa yatakupata ambayo hutaweza kujiepusha nayo. Balaa litakukumba ambalo hutaweza kulipinga; maangamizi yatakujia ghafla ambayo hujapata kamwe kuyaona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, mabaya yatakujia, usiyojua kuyalogoa; teso litakuangukia, usiloweza kujizindikia. Mara angamizo litakujia, usilolijua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hasara itakupata ambayo hautaweza kujiepusha nayo. Magumu yatakutokea ambayo hautaweza kuyapinga; maangamizi yatakufikia kwa rafla ambayo haujapata kuyaona hata kidogo.