Isaiah 47:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe umejichosha bure na washauri wako. Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe! Wao huzigawa mbingu sehemusehemu, huzichunguza nyota na kubashiri kila mwezi yatakayokupata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure! Wanajimu wako na waje mbele, wale watazama nyota watabiriao mwezi baada ya mwezi, wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe umejichosha bure na washauri wako. Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe! Wao huzigawa mbingu sehemusehemu, huzichunguza nyota na kubashiri kila mwezi yatakayokupata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure! Wanajimu wako na waje mbele, wale watazamao nyota na watabirio mwezi baada ya mwezi, wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure! Wanajimu wako na waje mbele, wale watazama nyota watabiriao mwezi baada ya mwezi, wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wanajimu, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe umejichosha bure na washauri wako. Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe! Wao huzigawa mbingu sehemusehemu, huzichunguza nyota na kubashiri kila mwezi yatakayokupata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umechokeshwa na mashauri yako mengi; sasa na watokee, wakuokoe, wao waaguliao ya mbinguni nao wachunguzao nyota, wao waliolinganya kila mwandamo wa mwezi upande, yatakakotokea mabaya yatakayokujia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe umejichokesha bure na washauri wako. Basi, wajitokeze hao wenye akili wakuokoe! Wao wanagawanya mbingu sehemusehemu, wanachunguza nyota na kutabiri kila mwezi yatakayokupata.