Isaiah 47:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kumbuka, wao ni kama mabua makavu: Moto utayateketezea mbali! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika wako kama mabua makavu; moto utawateketeza. Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe kutokana na nguvu za mwali wa moto. Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto; hapa hakuna moto wa kuota.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kumbuka, wao ni kama mabua makavu: moto utayateketezea mbali! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika wako kama mabua makavu, moto utawateketeza. Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe kutokana na nguvu za mwali wa moto. Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu ye yote joto; hapa hakuna moto wa kuota.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika wako kama mabua makavu; moto utawateketeza. Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe kutokana na nguvu za mwali wa moto. Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto; hapa hakuna moto wa kuota.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa kutoka kwa nguvu za muali wa moto; hili halitakuwa kaa la kujipasha moto, wala moto wa kuota.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kumbuka, wao ni kama mabua makavu: Moto utayateketezea mbali! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watazameni! Wako kama makapi yaliyounguzwa na moto, hawawezi kujiokoa wenyewe katika moto uwashikao, hakuna makaa ya kuyaotea, wala hakuna jiko lenye moto la kukaa hapohapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao ni kama majani yenye kukauka: moto utayateketeza! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!