Isaiah 47:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’, nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea, wala kufikiri mwisho wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukasema, ‘Nitaendelea kuwa malkia milele!’ Lakini hukutafakari mambo haya wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukasema, Mimi nitakuwa bibi milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’, nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea, wala kufikiri mwisho wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukasema, ‘Nitaendelea kuwa malkia milele!’ Lakini hukutafakari mambo haya wala hukuwaza juu ya kile ambacho kingeweza kutokea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukasema, ‘Nitaendelea kuwa malkia milele!’ Lakini hukutafakari mambo haya wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukasema, Mimi nitakuwa malkia milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’, nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea, wala kufikiri mwisho wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukasema kwamba: Kale na kale nitakuwa mfalme! Kwa hiyo hukuyawaza hayo moyoni, wala hukukumbuka, ya kuwa yako na mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukasema, Mimi nitakuwa bibi milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulijisemesha ndani ya moyo: “Nitakuwa malkia milele”, nawe haukufikiri juu ya mambo yanayotokea, wala kuwaza juu ya mwisho wake.