Isaiah 47:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa, wewe unayedhani kuwa u salama, na kujisemea: ‘Ni mimi tu, na hakuna mwingine isipokuwa mimi. Kamwe sitakuwa mjane, wala sitafiwa na wanangu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa, ukaaye mahali pako pa salama, na kujiambia mwenyewe, ‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu. Kamwe sitakuwa mjane, wala sitafiwa na watoto.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi mfano wa mjane, wala sitajua kufiwa na watoto;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa, wewe unayedhani kuwa u salama, na kujisemea: ‘Ni mimi tu, na hakuna mwingine isipokuwa mimi. Kamwe sitakuwa mjane, wala sitafiwa na wanangu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa, ukaaye katika mahali pako pa salama na kujiambia mwenyewe, ‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu. Kamwe sitakuwa mjane wala sitafiwa na watoto.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa, ukaaye mahali pako pa salama, na kujiambia mwenyewe, ‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu. Kamwe sitakuwa mjane, wala sitafiwa na watoto.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi kama mjane, wala sitajua kufiwa na watoto;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa, wewe unayedhani kuwa u salama, na kujisemea: ‘Ni mimi tu, na hakuna mwingine isipokuwa mimi. Kamwe sitakuwa mjane, wala sitafiwa na wanangu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa yasikie haya, wewe mcheshi uliyekaa salama, uliyesema moyoni mwako: Ni mimi, hakuna mwingine tena! Sitakaa ujane, wala sitakujua kuwa pasipo watoto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi mfano wa mjane, wala sitajua kufiwa na watoto;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, basi, sikiliza, ewe mupenda raha, wewe unayezani kuwa katika usalama, na kujisemesha: Mimi ndiye. Hakuna mwingine isipokuwa mimi. Sitakuwa mujane hata kidogo, wala sitakufiwa na watoto wangu.