Isaiah 48:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikilizeni, enyi watu wa Yakobo, enyi mnaojulikana kwa jina la Israeli, nyinyi mlio wa ukoo wa Yuda. Nyinyi huapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kudai mnamwabudu Mungu wa Israeli; lakini hayo si ukweli wala sawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo, ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli, na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, ninyi mnaoapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mnaomwomba Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli au kwa haki;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda; mnaoapa kwa jina la Bwana, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikilizeni, enyi watu wa Yakobo, enyi mnaojulikana kwa jina la Israeli, nyinyi mlio wa ukoo wa Yuda. Nyinyi huapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kudai mnamwabudu Mungu wa Israeli; lakini hayo si ukweli wala sawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sikilizeni hili, Ee nyumba ya Yakobo, ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, ninyi mnaoapa kwa jina la BWANA, mnaomwomba Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli au kwa haki;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo, ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli, na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, ninyi mnaoapa kwa jina la bwana, mnaomwomba Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli au kwa haki;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda; mnaoapa kwa jina la BWANA, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikilizeni, enyi watu wa Yakobo, enyi mnaojulikana kwa jina la Israeli, nyinyi mlio wa ukoo wa Yuda. Nyinyi huapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kudai mnamwabudu Mungu wa Israeli; lakini hayo si ukweli wala sawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yasikieni haya, ninyi wa mlango wa Yakobo! Mnajiita kwa jina la Isiraeli, mlitoka viunoni mwa Yuda, mnaapa na kulitaja Jina la Bwana, naye Mungu wa Isiraeli mnamtukuza; lakini si kwa kweli wala kwa wongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda; mnaoapa kwa jina la BWANA, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize, enyi watu wa Yakobo, enyi munaojulikana kwa jina la Israeli, ninyi munaokuwa wa uzao wa Yuda. Ninyi munaapa kwa jina la Yawe, na kudai kwamba munamwabudu Mungu wa Israeli; lakini hayo si ukweli wala sawa.