Isaiah 48:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli, Mkombozi wako, asema hivi: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ninayekufundisha kwa faida yako, ninayekuongoza katika njia unayotakiwa kwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli, Mkombozi wako, asema hivi: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ninayekufundisha kwa faida yako, ninayekuongoza katika njia unayotakiwa kwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Mimi ni bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli, Mkombozi wako, asema hivi: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ninayekufundisha kwa faida yako, ninayekuongoza katika njia unayotakiwa kwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, anavyosema Bwana aliyekukomboa, aliye Mtakatifu wa Isiraeli: Mimi Bwana ndimi Mungu wako; ninakufundisha yafaayo, ninakuongoza katika njia, utakayoishika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mutakatifu wa Israeli, Mukombozi wako, anasema hivi: Mimi ndiye Yawe, Mungu wako; ninayekufundisha kwa faida yako na kukuongoza katika njia unayotakiwa kwenda.