Isaiah 48:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo nilikutangazia tangu zamani, kabla hayajatukia mimi nilikutangazia, usije ukasema, ‘Kinyago changu kiliyatenda hayo, sanamu zangu za kuchonga na kusubu ziliyafanya.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani, kabla hayajatokea nilikutangazia ili usije ukasema, ‘Sanamu zangu zilifanya hayo; sanamu yangu ya mti, na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi nimekuonyesha tangu zamani; kabla hayajatukia nalikuonyesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo nilikutangazia tangu zamani, kabla hayajatukia mimi nilikutangazia, usije ukasema, ‘Kinyago changu kiliyatenda hayo, sanamu zangu za kuchonga na kusubu ziliyafanya.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani, kabla hayajatokea nilikutangazia ili kwamba usije ukasema, ‘Sanamu zangu zilifanya hayo; kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma ameyaamuru.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani, kabla hayajatokea nilikutangazia ili usije ukasema, ‘Sanamu zangu zilifanya hayo; kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi nimekuonesha tangu zamani; kabla hayajatukia nilikuonesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo nilikutangazia tangu zamani, kabla hayajatukia mimi nilikutangazia, usije ukasema, ‘Kinyago changu kiliyatenda hayo, sanamu zangu za kuchonga na kusubu ziliyafanya.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikakutangazia hapo kale, nikakuambia uyasikie, yalipokuwa hayajatimia bado, usiseme: Kinyago changu kimeyafanya! wala: Kinyago changu cha mti uliochongwa au cha shaba iliyoyeyushwa kimeyaagiza!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi nimekuonyesha tangu zamani; kabla hayajatukia nalikuonyesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo nilikutangazia mambo yale tangu zamani, mbele hayajatukia, mimi nilikujulisha, kusudi usiseme: Ni sanamu yangu iliyotenda mambo hayo, sanamu zangu za chuma ndizo ziliyaagiza.