Isaiah 49:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nisikilizeni, enyi nchi za mbali, tegeni sikio, enyi watu wa mbali! Mwenyezi-Mungu aliniita kabla sijazaliwa, alitaja jina langu nikiwa tumboni mwa mama yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwa, Mwenyezi Mungu aliniita, tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nisikilizeni, enyi nchi za mbali, tegeni sikio, enyi watu wa mbali! Mwenyezi-Mungu aliniita kabla sijazaliwa, alitaja jina langu nikiwa tumboni mwa mama yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nisikilizeni, Enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwa BWANA aliniita, tangu kuzaliwa kwangu amelitaja jina langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwa, bwana aliniita, tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nisikilizeni, enyi nchi za mbali, tegeni sikio, enyi watu wa mbali! Mwenyezi-Mungu aliniita kabla sijazaliwa, alitaja jina langu nikiwa tumboni mwa mama yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nisikieni, ninyi visiwa, nanyi makabila ya watu mlioko mbali, tegeni masikio! Bwana aliniita hapo nilipozaliwa, akalikuza jina langu tangu hapo, nilipotoka tumboni mwa mama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munisikilize, enyi inchi za mbali, Mutege sikio, enyi watu wa mbali! Yawe aliniita mbele sijazaliwa, alitaja jina langu nikiwa katika tumbo la mama yangu.