Isaiah 49:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawataona tena njaa wala kuwa na kiu. Upepo wa hari wala jua havitawachoma, mimi niliyewahurumia nitawaongoza na kuwapeleka kwenye chemchemi za maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawataona njaa wala kuona kiu, wala hari ya jangwani au jua halitawapiga. Yeye mwenye huruma juu yao atawaonesha njia, na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawataona tena njaa wala kuwa na kiu. Upepo wa hari wala jua havitawachoma, mimi niliyewahurumia nitawaongoza na kuwapeleka kwenye chemchemi za maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawataona njaa wala kuona kiu, wala hari ya jangwani au jua halitawapiga. Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawataona njaa wala kuona kiu, wala hari ya jangwani au jua halitawapiga. Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia, na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hawataona njaa, wala hawataona kiu; joto halitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawataona tena njaa wala kuwa na kiu. Upepo wa hari wala jua havitawachoma, mimi niliyewahurumia nitawaongoza na kuwapeleka kwenye chemchemi za maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawataona tena njaa wala kiu, hawatapigwa na upepo wenye joto wala na jua, kwani awahurumiaye atawaongoza, awapeleke kwenye visima vya maji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawatasikia tena njaa wala kuwa na kiu. Upepo wenye kuunguza wala jua havitawachoma, mimi niliyewahurumia nitawaongoza na kuwapeleka kwenye chemichemi za maji.