Isaiah 49:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya, asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake? Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe, mimi kamwe sitakusahau.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, mama aweza kumsahau mtoto aliye matitini mwake akinyonya, wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, mimi sitakusahau wewe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya, asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake? Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe, mimi kamwe sitakusahau.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, mama aweza kumsahau mtoto aliyeko matitini mwake akinyonya, wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, mimi sitakusahau wewe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, mama aweza kumsahau mtoto aliyeko matitini mwake akinyonya, wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, mimi sitakusahau wewe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya, asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake? Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe, mimi kamwe sitakusahau.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Mwanamke humsahau mtoto wake mnyonyaji, asimhurumie mwana, aliyemzaa? Ijapo amsahau, mimi sitakusahau kamwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe anasema: Munafikiri kwamba mama anaweza kumusahau mutoto anayemunyonyesha, wala kumuchukia mutoto wa tumbo lake? Hata kama mama anaweza kumusahau mutoto wake, mimi sitakusahau hata kidogo.