Isaiah 49:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inua macho uangalie pande zote; watu wako wote wanakusanyika na kukujia. Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu, watu wako watakuwa kwako kama mapambo, utawafurahia kama afanyavyo bibi arusi na utaji wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inua macho yako ukatazame pande zote: wana wako wote wanakusanyika na kukujia. Kwa hakika kama vile niishivyo, utawavaa wote kama mapambo, na kujifunga nao kama bibi arusi,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema Bwana, hakika utajivika na hao wote, kama kwa uzuri, nawe utajifungia hao, kama bibi arusi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inua macho uangalie pande zote; watu wako wote wanakusanyika na kukujia. Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu, watu wako watakuwa kwako kama mapambo, utawafurahia kama afanyavyo bibi arusi na utaji wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Inua macho yako ukatazame pande zote, wana wako wote wanakusanyika na kukujia. Kwa hakika kama vile niishivyo, utawavaa wote kama mapambo, na kujifunga nao kama bibi arusi,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inua macho yako ukatazame pande zote: wana wako wote wanakusanyika na kukujia. Kwa hakika kama vile niishivyo, utawavaa wote kama mapambo, na kujifunga nao kama bibi arusi,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema BWANA, hakika utajivika hao wote kama pambo, nawe utajipamba kwao kama bibi harusi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inua macho uangalie pande zote; watu wako wote wanakusanyika na kukujia. Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu, watu wako watakuwa kwako kama mapambo, utawafurahia kama afanyavyo bibi arusi na utaji wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yainue macho yako na kuyazungusha, uone! Hawa wote wamekusanyika, wafike kwako! Ndivyo, asemavyo Bwana: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, hawa wote utawavaa kama mapambo, utawatumia kuwa kama ukanda wa mchumba mke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema BWANA, hakika utajivika na hao wote, kama kwa uzuri, nawe utajifungia hao, kama bibi arusi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inua macho uangalie pande zote; watu wako wote wanakusanyika na kukufikia. Kama vile ninavyoishi, watu wako watakuwa kwako kama mapambo, utawafurahia kama vile bibi arusi anavyofanya na taji lake. –Ni ujumbe wa Yawe.