Isaiah 49:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kweli umekumbana na uharibifu, makao yako yamekuwa matupu, na nchi yako imeteketezwa. Lakini sasa itakuwa ndogo mno kwa wakazi wake; na wale waliokumaliza watakuwa mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa, na nchi yako ikaharibiwa, sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako, nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana katika habari za mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kweli umekumbana na uharibifu, makao yako yamekuwa matupu, na nchi yako imeteketezwa. Lakini sasa itakuwa ndogo mno kwa wakazi wake; na wale waliokumaliza watakuwa mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa na nchi yako ikaharibiwa, sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako, nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa, na nchi yako ikaharibiwa, sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako, nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kuhusu mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kweli umekumbana na uharibifu, makao yako yamekuwa matupu, na nchi yako imeteketezwa. Lakini sasa itakuwa ndogo mno kwa wakazi wake; na wale waliokumaliza watakuwa mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mahame na mapori yako na mashamba yako yaliyokufa sasa hayatawaeneza watakaokuja, wakae, nao waliokumeza watakuwa wamekwenda mbali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana katika habari za mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli umepatwa na uharibifu, makao yako yamekuwa matupu, na inchi yako imeteketezwa. Lakini sasa itakuwa ndogo sana kwa wakaaji wake.