Isaiah 49:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliyapa ukali maneno yangu kama upanga mkali, alinificha katika kivuli cha mkono wake; aliufanya ujumbe wangu mkali kama ncha ya mshale, akanificha katika podo lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa, na kunificha katika podo lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliyapa ukali maneno yangu kama upanga mkali, alinificha katika kivuli cha mkono wake; aliufanya ujumbe wangu mkali kama ncha ya mshale, akanificha katika podo lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa na kunificha katika podo lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa, na kunificha katika podo lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliyapa ukali maneno yangu kama upanga mkali, alinificha katika kivuli cha mkono wake; aliufanya ujumbe wangu mkali kama ncha ya mshale, akanificha katika podo lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akakitumikisha kinywa changu kama upanga mkali, akanificha kivulini mwa mkono wake, akanitumia kuwa mshale umetukao, akanificha katika podo lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifanya maneno yangu kuwa makali kama upanga mukali, alinificha katika kivuli cha mukono wake; aliufanya ujumbe wangu kuwa mukali kama chongo ya mushale, akanificha kama mushale ndani ya mufuko wake.