Isaiah 49:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana Mungu asema hivi: “Nitayapungia mkono mataifa; naam, nitayapa ishara, nayo yatawabeba watoto wenu wa kiume, kadhalika na watoto wenu wa kike na kuwarudisha kwako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa, nitainua bendera yangu kwa mataifa; watawaleta wana wako mikononi yao, na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana Mungu asema hivi: “Nitayapungia mkono mataifa; naam, nitayapa ishara, nayo yatawabeba watoto wenu wa kiume, kadhalika na watoto wenu wa kike na kuwarudisha kwako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi: “Tazama, nitawaashiria watu Mataifa, nitainua bendera yangu kwa mataifa; watawaleta wana wako kwenye mikono yao na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana Mwenyezi: “Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa, nitainua bendera yangu kwa mataifa; watawaleta wana wako mikononi yao, na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwainulia makabila ya watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana Mungu asema hivi: “Nitayapungia mkono mataifa; naam, nitayapa ishara, nayo yatawabeba watoto wenu wa kiume, kadhalika na watoto wenu wa kike na kuwarudisha kwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Tazama! Nitawapungia wamizimu kwa mkono wangu, nitawatwekea makabila ya watu bendera yangu; ndipo, watakapowaleta wanao na kuwabeba vifuani, nao watoto wako wa kike watawachukua mabegani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitasimika bendera kwa kuita mataifa; nitayaonyesha kitambulisho. Nayo yatawarudishia wana wenu wakiwabeba kwenye kifua, vilevile na wabinti zenu kwenye mabega.