Isaiah 49:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafalme watakushughulikia, na malkia watakutengenezea chakula. Watakusujudia na kukupa heshima, na kuramba vumbi iliyo miguuni pako. Hapo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu; wote wanaonitegemea hawataaibika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea, na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea. Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa chini; wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako. Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu; wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena waningojeao hawatatahayarika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafalme watakushughulikia, na malkia watakutengenezea chakula. Watakusujudia na kukupa heshima, na kuramba vumbi iliyo miguuni pako. Hapo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu; wote wanaonitegemea hawataaibika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea. Watasujudu mbele yako na nyuso zao zikigusa ardhi; watalamba mavumbi yaliyo miguuni mwako. Ndipo utajua yakuwa Mimi ndimi BWANA; wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea, na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea. Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi; wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako. Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi bwana; wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafalme watakushughulikia, na malkia watakutengenezea chakula. Watakusujudia na kukupa heshima, na kuramba vumbi iliyo miguuni pako. Hapo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu; wote wanaonitegemea hawataaibika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafalme watakuwa walezi wako, nao wake wa kifalme watakuwa wanyonyeshaji wako, watakuangukia kifudifudi, walambe mavumbi miguuni pako; ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, ya kuwa hawapatwi na soni waningojeao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafalme watakushugulikia, na malkia watakutengenezea chakula. Watainama mbele yako uso mpaka chini, na kulambula mavumbi ya miguu yako. Halafu utatambua kwamba mimi ni Yawe; wote wanaonitegemea hawatapata haya.