Isaiah 49:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ajibu: “Naam! Hata nyara za shujaa zitachukuliwa, mateka wa mtu katili wataokolewa. Mimi mwenyewe nitawakabili maadui zako, mimi mwenyewe nitawaokoa watoto wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa, na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali. Nitashindana na wale wanaoshindana nawe, nami nitawaokoa watoto wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ajibu: “Naam! Hata nyara za shujaa zitachukuliwa, mateka wa mtu katili wataokolewa. Mimi mwenyewe nitawakabili maadui zako, mimi mwenyewe nitawaokoa watoto wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hili ndilo asemalo BWANA: “Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa, na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali. Nitashindana na wale wanaoshindana nawe, nami nitawaokoa watoto wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hili ndilo asemalo bwana: “Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa, na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali. Nitashindana na wale wanaoshindana nawe, nami nitawaokoa watoto wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, BWANA asema hivi, Hata mateka wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka wake aliye katili wataokoka; kwa maana nitapambana na yeye abishanaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ajibu: “Naam! Hata nyara za shujaa zitachukuliwa, mateka wa mtu katili wataokolewa. Mimi mwenyewe nitawakabili maadui zako, mimi mwenyewe nitawaokoa watoto wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kweli nazo kole za mwenye nguvu zitachukuliwa, nayo mateka ya mkorofi yatapona; maana wao waliokugombeza nitawagombeza mimi, nao wanao nitawaokoa mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, BWANA asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kweli! Hata mateka za shujaa zitarudishwa, wafungwa wa mutu mutesaji wataokolewa. Mimi mwenyewe nitawapiganisha waadui zako, mimi mwenyewe nitawaokoa watoto wako.