Isaiah 49:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawafanya wanaokukandamiza watafunane; watalewa damu yao wenyewe kama divai. Hapo binadamu wote watatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mwokozi wako, mimi ni Mkombozi wako, Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawafanya wanaokudhulumu wale nyama yao wenyewe; watalewa kwa damu yao wenyewe, kama vile kwa mvinyo. Ndipo wanadamu wote watajua ya kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, ni Mwokozi wako, Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawafanya wanaokukandamiza watafunane; watalewa damu yao wenyewe kama divai. Hapo binadamu wote watatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mwokozi wako, mimi ni Mkombozi wako, Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe, watalewa kwa damu yao wenyewe, kama vile kwa mvinyo. Ndipo wanadamu wote watajua ya kuwa Mimi, BWANA, ni Mwokozi wako, Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe, watalewa kwa damu yao wenyewe, kama vile kwa mvinyo. Ndipo wanadamu wote watajua ya kuwa Mimi, bwana, ni Mwokozi wako, Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na watu wote watajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawafanya wanaokukandamiza watafunane; watalewa damu yao wenyewe kama divai. Hapo binadamu wote watatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mwokozi wako, mimi ni Mkombozi wako, Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliokutesa nitawalisha nyama zao, wanywe damu zao kama ni pombe, mpaka walewe; ndipo, wote wenye miili ya kimtu watakapojua, ya kuwa mimi ndimi Bwana, mwokozi wako, ni mkombozi wako akutawalaye, Yakobo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawasukuma watesaji wako wakule miili yao wenyewe; watalewa damu yao wenyewe kama divai. Halafu wanadamu wote watatambua kwamba mimi ni Yawe, Mwokozi wako, Mukombozi wako, Mwenye Nguvu wa Yakobo.