Isaiah 49:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini asema sasa Mwenyezi-Mungu, ambaye aliniita tangu tumboni mwa mama yangu ili nipate kuwa mtumishi wake; nilirudishe taifa la Yakobo kwake, niwakusanye wazawa wa Israeli kwake. Mwenyezi-Mungu amenijalia heshima mbele yake. Mungu wangu amekuwa ndiye nguvu yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa Mwenyezi Mungu asema: yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake, kumrudisha tena Yakobo kwake na kumkusanyia Israeli, kwa maana nimepata heshima machoni pa Mwenyezi Mungu, naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu);
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini asema sasa Mwenyezi-Mungu, ambaye aliniita tangu tumboni mwa mama yangu ili nipate kuwa mtumishi wake; nilirudishe taifa la Yakobo kwake, niwakusanye wazawa wa Israeli kwake. Mwenyezi-Mungu amenijalia heshima mbele yake. Mungu wangu amekuwa ndiye nguvu yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa BWANA asema, yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake kumrudisha tena Yakobo kwake na kumkusanyia Israeli, kwa maana nimepata heshima machoni pa BWANA, naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa bwana asema: yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake, kumrudisha tena Yakobo kwake na kumkusanyia Israeli, kwa maana nimepata heshima machoni pa bwana, naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa BWANA asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya BWANA, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu);
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini asema sasa Mwenyezi-Mungu, ambaye aliniita tangu tumboni mwa mama yangu ili nipate kuwa mtumishi wake; nilirudishe taifa la Yakobo kwake, niwakusanye wazawa wa Israeli kwake. Mwenyezi-Mungu amenijalia heshima mbele yake. Mungu wangu amekuwa ndiye nguvu yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nimeambiwa neno na Bwana aliyenitengeneza tumboni mwa mama kuwa mtumishi wake wa kumrudisha Yakobo kwake, Waisiraeli wapate kukusanyika kwake; kwani nimetukuka machoni pa Bwana, Mungu wangu akawa nguvu zangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa BWANA asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya BWANA, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu);
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa Yawe anasema. Aliniita tangu katika tumbo la mama kusudi nipate kuwa mutumishi wake, nilirudishe taifa la Yakobo kwake na kukusanya wazao wa Israeli kwake. Yawe amenijalia heshima mbele yake. Mungu wangu amekuwa nguvu yangu.