Isaiah 49:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye asema: “Haitoshi tu wewe kuwa mtumishi wangu, uyainue makabila ya Yakobo, na kurekebisha watu wa Israeli waliobaki. Nitakufanya uwe mwanga wa mataifa, niwaletee wokovu watu wote duniani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yeye asema: “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kurejesha makabila ya Yakobo, na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa, ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye asema: “Haitoshi tu wewe kuwa mtumishi wangu, uyainue makabila ya Yakobo, na kurekebisha watu wa Israeli waliobaki. Nitakufanya uwe mwanga wa mataifa, niwaletee wokovu watu wote duniani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
anasema: “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kurejeza upya makabila ya Yakobo, na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu Mataifa, ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeye asema: “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kurejeza makabila ya Yakobo, na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa, ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye asema: “Haitoshi tu wewe kuwa mtumishi wangu, uyainue makabila ya Yakobo, na kurekebisha watu wa Israeli waliobaki. Nitakufanya uwe mwanga wa mataifa, niwaletee wokovu watu wote duniani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amesema hivi: Haitoshi, ukiwa mtumishi wangu wa kuiinua milango ya Yakobo na wa kuwarudisha Waisiraeli waliookoka, nimekuweka tena kuwa mwanga wa wamizimu, wokovu wangu ufike mapeoni kwa nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye anasema: Haitoshi tu wewe kuwa mutumishi wangu, kusudi uyainue makabila ya Yakobo, na kurudisha watu wa Israeli waliobaki. Nitakufanya ukuwe mwangaza wa mataifa, kusudi watu wote wapate kuokolewa katika dunia.