Isaiah 5:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanakondoo, wanambuzi na ndama, watapata malisho yao kwenye magofu ya miji yao, kana kwamba hizo ni sehemu za malisho yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe, wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wana-kondoo watakapolisha kama katika malisho yao wenyewe, na mahali pao waliowanda, palipoachwa ukiwa, wageni watakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanakondoo, wanambuzi na ndama, watapata malisho yao kwenye magofu ya miji yao, kana kwamba hizo ni sehemu za malisho yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe, wana-kondoo na wageni watajilisha katika magofu ya matajiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe, wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wana-kondoo watakapojilisha kama walio katika malisho yao wenyewe, na mahali pao walionenepa, palipoachwa ukiwa, wageni watakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanakondoo, wanambuzi na ndama, watapata malisho yao kwenye magofu ya miji yao, kana kwamba hizo ni sehemu za malisho yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa kondoo watalisha hapo, kama ni malisho yao, nako kwenye mahame ya wale wakwasi watakula wageni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wana-kondoo watakapolisha kama katika malisho yao wenyewe, na mahali pao waliowanda, palipoachwa ukiwa, wageni watakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wana-kondoo watakula majani kule, kama vile katika shamba la kuwakulishia. Wana-mbuzi wanono watatafuta chakula chao kule kule.