Isaiah 5:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwawakia watu wake, akaunyosha mkono wake dhidi yao, akawachapa, hata milima ikatetemeka, maiti zao zikawa kama takataka katika barabara za mji. Hata hivyo, hasira yake haikutulia, mkono wake bado ameunyosha kuwaadhibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi Mungu inawaka dhidi ya watu wake, mkono wake umeinuliwa na anawapiga. Milima inatetemeka, maiti ni kama takataka kwenye barabara. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo hasira ya Bwana imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwawakia watu wake, akaunyosha mkono wake dhidi yao, akawachapa, hata milima ikatetemeka, maiti zao zikawa kama takataka katika barabara za mji. Hata hivyo, hasira yake haikutulia, mkono wake bado ameunyosha kuwaadhibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hasira ya BWANA inawaka dhidi ya watu wake, mkono wake umeinuliwa na anawapiga. Milima inatetemeka, maiti ni kama takataka kwenye barabara. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hasira ya bwana inawaka dhidi ya watu wake, mkono wake umeinuliwa na anawapiga. Milima inatetemeka, maiti ni kama takataka kwenye barabara. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwawakia watu wake, akaunyosha mkono wake dhidi yao, akawachapa, hata milima ikatetemeka, maiti zao zikawa kama takataka katika barabara za mji. Hata hivyo, hasira yake haikutulia, mkono wake bado ameunyosha kuwaadhibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana akawachafukia walio ukoo wake, mkono wake ukawainamia, ukawapiga; milima ikatetemeka, mizoga yao ikawa kama mataka njiani. Kwa hayo yote makali yake hayajatulia bado, mkono wake ungaliko umekunjuka bado.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo hasira ya Yawe iliwawakia watu wake, akaunyoosha mukono wake juu yao, akawaazibu. Milima ikatetemeka, maiti zao zikakuwa kama takataka katika barabara za muji. Hata hivyo, hasira yake haijatulia, angali ananyoosha mukono wake kwa kuwaazibu.