Isaiah 5:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mishale yao ni mikali, pinde zao zote zimevutwa, kwato za farasi wao ziko kama gumegume, magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika; Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mishale yao ni mikali, pinde zao zote zimevutwa, kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume, magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mishale yao ni mikali, pinde zao zote zimevutwa, kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume, magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mishale yao ni mikali, na pinde zao zote zimepindika; Kwato za farasi wao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mishale yao itakuwa imenolewa, nyuta zao zitakuwa zimepindwa, kwato za farasi wao zitaonekana kuwa ngumu kama mawe, magurudumu ya magari yao yatapiga mbio kama upepo mkali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika; Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kama wa upepo mukali.