Isaiah 5:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Askari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama wanasimba ambao wamekamata mawindo yao na kuwapeleka mahali mbali ambapo hakuna awezaye kuwanyanganya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ngurumo yao ni kama ile ya simba, wananguruma kama wana simba, wanakoroma wanapokamata mawindo yao, na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wana-simba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Askari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama wanasimba ambao wamekamata mawindo yao na kuwapeleka mahali mbali ambapo hakuna awezaye kuwanyang'anya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ngurumo yao ni kama ile ya simba, wananguruma kama wana simba, wanakoroma wanapokamata mawindo yao na kuondoka nayo pasipo ye yote wa kuokoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ngurumo yao ni kama ile ya simba, wananguruma kama wana simba, wanakoroma wanapokamata mawindo yao, na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Askari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama wanasimba ambao wamekamata mawindo yao na kuwapeleka mahali mbali ambapo hakuna awezaye kuwanyanganya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mazomeo yao ni kama ngurumo ya simba, hulia kama wana wa simba. Watakuja na kuvuma na kukamata mateka, wayapeleke kwao; napo hapo hatakuwapo atakayewaponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wana-simba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama simba wakali ambao wamekamata nyama wao na kuwapeleka mbali ambapo hakuna anayeweza kuwanyanganya.