Isaiah 5:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam! Shamba la mizabibu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi ni jumuiya ya Waisraeli, na mizabibu mizuri aliyoipanda ni watu wa Yuda. Yeye alitazamia watende haki, badala yake wakafanya mauaji; alitazamia uadilifu, badala yake wakasababisha kilio!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shamba la mzabibu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ni nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni bustani yake ya kumpendeza. Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu; alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam! Shamba la mizabibu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi ni jumuiya ya Waisraeli, na mizabibu mizuri aliyoipanda ni watu wa Yuda. Yeye alitazamia watende haki, badala yake wakafanya mauaji; alitazamia uadilifu, badala yake wakasababisha kilio!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shamba la mzabibu la BWANA Mwenye Nguvu Zote ni nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni bustani yake ya kumpendeza. Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu, alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shamba la mzabibu la bwana Mwenye Nguvu Zote ni nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni bustani yake ya kumpendeza. Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu, alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam! Shamba la mizabibu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi ni jumuiya ya Waisraeli, na mizabibu mizuri aliyoipanda ni watu wa Yuda. Yeye alitazamia watende haki, badala yake wakafanya mauaji; alitazamia uadilifu, badala yake wakasababisha kilio!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mizabibu ya Bwana Mwenye vikosi ni mlango wa Isiraeli na watu wa Yuda, ndio shamba lake lipendwalo naye. Akangojea manyofu, lakini alipotazama, ni mapotovu; akangojea wongofu, lakini alipotazama, ni vilio tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Shamba la mizabibu la Yawe wa majeshi ni taifa la Waisraeli, na mizabibu mizuri aliyoipanda ni watu wa Yuda. Yeye alitazamia watu wafuate sheria yake, akaona mauaji; alitazamia haki, alisikia kilio!