Isaiah 5:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wao wanaonunua nyumba baada ya nyumba, wanaoongeza mashamba juu ya mashamba yao, mpaka kila sehemu inakuwa mali yao, na hamna nafasi kwa wengine nchini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba na kuunganisha mashamba baada ya mashamba hadi hakuna nafasi iliyobaki, nanyi mnaishi peke yenu katika nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena, nanyi hamna budi kukaa peke yenu kati ya nchi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wao wanaonunua nyumba baada ya nyumba, wanaoongeza mashamba juu ya mashamba yao, mpaka kila sehemu inakuwa mali yao, na hamna nafasi kwa wengine nchini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba na kuunganisha mashamba baada ya mashamba hadi hakuna nafasi iliyobaki nanyi mnaishi peke yenu katika nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba na kuunganisha mashamba baada ya mashamba hadi hakuna nafasi iliyobaki, nanyi mnaishi peke yenu katika nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hadi ikawa hapana nafasi tena, nanyi ikawa hamna budi kukaa peke yenu katikati ya nchi!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wao wanaonunua nyumba baada ya nyumba, wanaoongeza mashamba juu ya mashamba yao, mpaka kila sehemu inakuwa mali yao, na hamna nafasi kwa wengine nchini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata wanaokusanya nyumba na nyumba ndio wanajiongezea mashamba na mashamba, pasiwepo tena mahali pasipo penu, mkae peke yenu katika nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena, nanyi hamna budi kukaa peke yenu kati ya nchi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwao wanaoongeza nyumba juu ya nyumba, wanaoongeza mashamba juu ya mashamba yao, mpaka kila sehemu inakuwa mali yao, na hakuna nafasi kwa wengine katika inchi.