Isaiah 50:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kama nimempa talaka mama yako Yerusalemu, hati ya talaka iko wapi? Au kama niliwauza utumwani, yuko wapi basi, huyo niliyemwuzia? Kumbukeni mliuzwa utumwani kwa maovu yenu, mama yenu alifukuzwa kwa makosa yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako ambayo kwayo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani miongoni mwa watu wanaonidai? Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kama nimempa talaka mama yako Yerusalemu, hati ya talaka iko wapi? Au kama niliwauza utumwani, yuko wapi basi, huyo niliyemwuzia? Kumbukeni mliuzwa utumwani kwa maovu yenu, mama yenu alifukuzwa kwa makosa yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako ambayo kwayo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani miongoni mwa watu wanaonidai? Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, kwa sababu ya makosa mama yenu aliachwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako ambayo kwayo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani miongoni mwa watu wanaonidai? Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kama nimempa talaka mama yako Yerusalemu, hati ya talaka iko wapi? Au kama niliwauza utumwani, yuko wapi basi, huyo niliyemwuzia? Kumbukeni mliuzwa utumwani kwa maovu yenu, mama yenu alifukuzwa kwa makosa yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kiko wapi cheti cha kuachana, nilichompa mama yenu nilipomtuma kujiendea? Au yuko nani aliyenidai, nikawauza ninyi kwake? Tazameni: Mmeuzwa kwa ajili ya manza zenu, mlizozikora; tena ni kwa ajili ya mapotovu yenu, mama yenu akitumwa kujiendea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kama nimeachana na mama yako Yerusalema, barua ya kuachana iko wapi? Nilikuwa na deni ya nani kwa kuwauzisha? Mukumbuke kwamba muliuzishwa kwa ajili ya maovu yenu, mama yenu alifukuzwa kwa ajili ya makosa yenu.