Isaiah 50:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi mnaowasha moto, na kujifanyia silaha za mienge, tembeeni kwa mwanga wa moto huo, miali ya moto mliowasha nyinyi wenyewe. Mtakachopata kutoka kwa Mwenyezi-Mungu ni hiki: Nyinyi mtalala chini na mateso makali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto, na kupeana mienge iwakayo ninyi kwa ninyi, nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu na ya mienge mliyoiwasha. Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu: Mtalala chini kwa mateso makali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi mnaowasha moto, na kujifanyia silaha za mienge, tembeeni kwa mwanga wa moto huo, miali ya moto mliowasha nyinyi wenyewe. Mtakachopata kutoka kwa Mwenyezi-Mungu ni hiki: nyinyi mtalala chini na mateso makali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto na kupeana ninyi kwa ninyi mienge iwakayo, nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu na ya mienge mliyoiwasha. Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu: Mtalala chini kwa mateso makali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto, na kupeana mienge iwakayo ninyi kwa ninyi, nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu na ya mienge mliyoiwasha. Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu: Mtalala chini kwa mateso makali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; nendeni ninyi katika muali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi mnaowasha moto, na kujifanyia silaha za mienge, tembeeni kwa mwanga wa moto huo, miali ya moto mliowasha nyinyi wenyewe. Mtakachopata kutoka kwa Mwenyezi-Mungu ni hiki: Nyinyi mtalala chini na mateso makali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa ninyi nyote mnaowasha moto, mwikoleze mishale ya moto, nendeni kuunguzwa na moto wenu, mishale, mliyoiwasha, iwachome moto! Hayo yatatokea mkononi mwangu, yawajie, mlazwe mahali panapoumiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi munaowasha moto, na kujifanyia silaha za mienge, mutembee kwa mwangaza wa moto huo, ndimi za moto muliowasha ninyi wenyewe. Kitu mutakachopata kutoka kwa Yawe ni hiki: ninyi mutalala chini na mateso makali.