Isaiah 50:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana Mungu hunisaidia, kwa hiyo siwezi kufadhaika. Uso wangu nimeukaza kama jiwe; najua kwamba sitaaibishwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu Bwana Mungu Mwenyezi ananisaidia, sitatahayarika. Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami ninajua sitaaibika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana Mungu hunisaidia, kwa hiyo siwezi kufadhaika. Uso wangu nimeukaza kama jiwe; najua kwamba sitaaibishwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu BWANA Mwenyezi ananisaidia, sitatahayarika. Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume, nami ninajua sitaaibika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu bwana Mwenyezi ananisaidia, sitatahayarika. Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume, nami ninajua sitaaibika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana Mungu hunisaidia, kwa hiyo siwezi kufadhaika. Uso wangu nimeukaza kama jiwe; najua kwamba sitaaibishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu akanisaidia, kwa hiyo sikutwezeka, kwa hiyo nikaushupaza uso wangu kuwa kama jiwe la moto, nikajua, ya kuwa sitaiva uso.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe ananisaidia kwa hiyo siwezi kufazaika. Uso wangu nimeukaza kama jiwe; ninajua kwamba sitapata haya.