Isaiah 50:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama Bwana Mungu hunisaidia. Ni nani awezaye kusema nina hatia? Maadui zangu wote watachakaa kama vazi, nondo watawatafuna.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni Bwana Mungu Mwenyezi anisaidiaye mimi. Ni nani huyo atakayenihukumu? Wote watachakaa kama vazi, nondo watawala wawamalize.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama Bwana Mungu hunisaidia. Ni nani awezaye kusema nina hatia? Maadui zangu wote watachakaa kama vazi, nondo watawatafuna.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni BWANA Mwenyezi ndiye anisaidiaye mimi. Ni nani huyo atakayenihukumu? Wote watachakaa kama vazi, nondo atawala awamalize.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi. Ni nani huyo atakayenihukumu? Wote watachakaa kama vazi, nondo watawala wawamalize.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mwenye hatia? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama Bwana Mungu hunisaidia. Ni nani awezaye kusema nina hatia? Maadui zangu wote watachakaa kama vazi, nondo watawatafuna.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na mwone, ya kuwa Bwana Mungu ananisaidia! Yuko nani atakayenishinda? Na mwone, ya kuwa hawa wote watachakaa kama nguo, ikiliwa na nondo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia Bwana wetu Yawe ananisaidia. Ni nani anayeweza kusema niko na kosa? Waadui zangu wote watachakaa kama nguo, nondo watawatafuna.