Isaiah 51:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe umenisahau mimi Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyezitandaza mbingu, na kuiweka misingi ya dunia! Wewe waendelea kuogopa siku zote, kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu wako, kwamba yuko tayari kukuangamiza! Lakini hasira yake itafika wapi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwamba mnamsahau Mwenyezi Mungu Muumba wenu, aliyezitanda mbingu na kuiweka misingi ya dunia, kwamba mnaishi katika hofu siku zote kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, ambaye nia yake ni kuangamiza? Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukamsahau Bwana, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo afanyapo tayari kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe umenisahau mimi Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyezitandaza mbingu, na kuiweka misingi ya dunia! Wewe waendelea kuogopa siku zote, kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu wako, kwamba yuko tayari kukuangamiza! Lakini hasira yake itafika wapi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwamba mnamsahau BWANA Muumba wenu, aliyezitanda mbingu na kuiweka misingi ya dunia, kwamba mnaishi katika hofu siku zote kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, ambaye nia yake ni kuangamiza? Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwamba mnamsahau bwana Muumba wenu, aliyezitanda mbingu na kuiweka misingi ya dunia, kwamba mnaishi katika hofu siku zote kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, ambaye nia yake ni kuangamiza? Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe umenisahau mimi Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyezitandaza mbingu, na kuiweka misingi ya dunia! Wewe waendelea kuogopa siku zote, kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu wako, kwamba yuko tayari kukuangamiza! Lakini hasira yake itafika wapi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umemsahau Bwana aliyekufanya, aliyezitanda mbingu, aliyezishikiza nchi, ukatetemeka siku zote pasipo kukoma kwa ajili ya makali yake anayekusonga, kwa kuwa alitaka kukuangamiza; na sasa makali yake aliyekusonga yako wapi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo afanyapo tayari kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe umenisahau mimi Yawe Muumba wako, niliyezitandaza mbingu, na kuiweka misingi ya dunia! Kwa sababu ya kasirani ya yule anayekutesa, unaendelea kuogopa siku zote kwamba yuko tayari kukuangamiza! Lakini hasira yake itafikia wapi?