Isaiah 51:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amka ewe Yerusalemu! Amka usimame wima! Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake, nawe umeinywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amka, amka! Simama, ee Yerusalemu, wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Mwenyezi Mungu kikombe cha ghadhabu yake, wewe uliyekunywa hata machujo yake, kikombe kile cha kunywea kiwafanyacho watu kuyumbayumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea, mkononi mwa Bwana, Kikombe cha hasira yake; Bakuli la kikombe cha kulevya-levya Umelinywea na kulimaliza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amka ewe Yerusalemu! Amka usimame wima! Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake, nawe umeinywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amka, amka! Simama, Ee Yerusalemu, wewe uliyekunywa kutoka katika mkono wa BWANA kikombe cha ghadhabu yake, wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake, kikombe kile cha kunywea kiwafanyacho watu kuyumbayumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amka, amka! Simama, ee Yerusalemu, wewe uliyekunywa kutoka mkono wa bwana kikombe cha ghadhabu yake, wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake, kikombe kile cha kunywea kiwafanyacho watu kuyumbayumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amka ewe Yerusalemu! Amka usimame wima! Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake, nawe umeinywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amka! Amka! Inuka, Yerusalemu! Umekunywa mkononi mwa Bwana kikombe chenye makali yake, hicho kikombe kilichojaa kileo cha kupepesusha umekinywa na kukimaliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea, mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Bakuli la kikombe cha kulevya-levya Umelinywea na kulimaliza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amuka, ewe Yerusalema! Amuka usimame wima! Yawe amekukunywesha kikombe cha kasirani yake, nawe umekikunywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.