Isaiah 51:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi: “Nimekuondolea kikombe cha kuyumbisha, hutakunywa tena kikombe cha ghadhabu yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi wako, Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake: “Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe kilichokufanya uyumbayumbe; kutoka kikombe hicho, kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu, kamwe hutakunywa tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi: “Nimekuondolea kikombe cha kuyumbisha, hutakunywa tena kikombe cha ghadhabu yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi wako, Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake: “Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe kilichokufanya uyumbeyumbe; kutoka katika kikombe hicho, kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu, kamwe hutakunywa tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana Mwenyezi wako, Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake: “Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe kilichokufanya uyumbayumbe; kutoka kikombe hicho, kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu, kamwe hutakunywa tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi: “Nimekuondolea kikombe cha kuyumbisha, hutakunywa tena kikombe cha ghadhabu yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, anavyosema Bwana aliye Bwana na Mungu wako, awapiganiaye walio ukoo wake: Tazama! Nimekichukua mkononi mwako kile kikombe chenye kileo cha kupepesusha, hicho kikombe kilichojaa makali yangu hutakinywa tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana, Yawe, Mungu wako, anayewatetea watu wake, anasema hivi: Nimekuondolea kikombe cha kuyumbisha, hautakunywa tena kikombe cha kasirani yangu.