Isaiah 51:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu nitaufariji mji wa Siyoni, nitaparekebisha mahali pake pote palipoharibika. Nyika zake nitazifanya kama bustani ya Edeni, majangwa yake kama bustani ya Mwenyezi-Mungu. Kwake kutapatikana furaha na shangwe, na nyimbo za shukrani zitasikika humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika Mwenyezi Mungu ataifariji Sayuni, naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote; atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni, nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya Mwenyezi Mungu. Shangwe na furaha zitakuwa ndani yake, shukrani na sauti za kuimba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nitaufariji mji wa Siyoni, nitaparekebisha mahali pake pote palipoharibika. Nyika zake nitazifanya kama bustani ya Edeni, majangwa yake kama bustani ya Mwenyezi-Mungu. Kwake kutapatikana furaha na shangwe, na nyimbo za shukrani zitasikika humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika BWANA ataifariji Sayuni naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote; atayafanya majangwa yake kama Edeni, nazo sehemu zake zisizolimika wala zisizofaa kukaliwa na watu kama bustani ya BWANA. Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake, shukrani na sauti za kuimba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika bwana ataifariji Sayuni, naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote; atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni, nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya bwana. Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake, shukrani na sauti za kuimba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya nyika yake kuwa kama bustani ya Edeni, na jangwa lake kama bustani ya BWANA; shangwe na furaha zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nitaufariji mji wa Siyoni, nitaparekebisha mahali pake pote palipoharibika. Nyika zake nitazifanya kama bustani ya Edeni, majangwa yake kama bustani ya Mwenyezi-Mungu. Kwake kutapatikana furaha na shangwe, na nyimbo za shukrani zitasikika humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana ameutuliza Sioni, ameyatuliza mabomoko yake yote, kwa kuwa atayageuza mapori yake kuwa mashamba, nazo nyika zake kuwa kama bustani ya Bwana. Ndipo, kutakapooneka mle kufurahi na kuchangamka, kushukuru na kuimba kwa sauti kuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya BWANA; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Yawe nitaufariji Sayuni, nitatengeneza pahali pake pote palipoharibika. Nitazifanya mbuga zake kama shamba la Edeni, jangwa yake kama bustani ya Yawe. Ndani yake kutapatikana furaha na shangwe, na nyimbo za shukrani zitasikilika humo.