Isaiah 51:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nisikilizeni enyi watu wangu, nitegeeni sikio enyi taifa langu. Sheria na haki zitatoka kwangu mimi; nazo zitakuwa mwanga wa mataifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nisikilizeni, watu wangu; nisikieni, taifa langu: Torati itatoka kwangu; haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, nami nitaistarehesha hukumu yangu iwe nuru ya mataifa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nisikilizeni enyi watu wangu, nitegeeni sikio enyi taifa langu. Sheria na haki zitatoka kwangu mimi; nazo zitakuwa mwanga wa mataifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nisikilizeni, watu wangu; nisikieni, taifa langu: Sheria itatoka kwangu; haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nisikilizeni, watu wangu; nisikieni, taifa langu: Sheria itatoka kwangu; haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, na kutoa haki yangu iwe nuru ya mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nisikilizeni enyi watu wangu, nitegeeni sikio enyi taifa langu. Sheria na haki zitatoka kwangu mimi; nazo zitakuwa mwanga wa mataifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Niangalieni, ninyi mlio ukoo wangu, ninyi mlio watu wangu nisikilizeni! Kwani maonyo yatatoka kwangu, nayo yanyokayo machoni pangu nitayaweka kuwa mwanga wa makabila ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, nami nitaistarehesha hukumu yangu iwe nuru ya mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munisikilize, enyi watu wangu, munitegee sikio, enyi taifa langu. Sheria na haki zitatoka kwangu mimi; nazo zitakuwa mwangaza wa mataifa.