Isaiah 51:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaleta ukombozi hima; wokovu nitakaoleta waanza kutokea. Mimi mwenyewe nitayatawala mataifa. Wakazi wa nchi za mbali wananingojea, wanaitegemea nguvu yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haki yangu inakaribia mbio, wokovu wangu unakuja, nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa. Visiwa vitanitegemea na kungojea mkono wangu kwa matumaini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu kabila za watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaleta ukombozi hima; wokovu nitakaoleta waanza kutokea. Mimi mwenyewe nitayatawala mataifa. Wakazi wa nchi za mbali wananingojea, wanaitegemea nguvu yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haki yangu inakaribia inakuja mbio, wokovu wangu unakuja, nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa. Visiwa vitanitegemea na kungojea kwa matumaini mkono wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haki yangu inakaribia mbio, wokovu wangu unakuja, nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa. Visiwa vitanitegemea na kungojea mkono wangu kwa matumaini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu makabila ya watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaleta ukombozi hima; wokovu nitakaoleta waanza kutokea. Mimi mwenyewe nitayatawala mataifa. Wakazi wa nchi za mbali wananingojea, wanaitegemea nguvu yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bado kidogo nitakuja kushinda na kuutokeza wokovu wangu; ndipo, mikono yangu itakapoyapatiliza makabila ya watu. Mimi ndimi, visiwa vitakayemngojea na kuuchungulia mkono wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu kabila za watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukombozi wangu unakaribia upesi; wokovu nitakaoleta unaanza kutokea. Mimi mwenyewe nitayatawala mataifa. Wakaaji wa inchi za mbali wananingojea, wanaitegemea nguvu yangu.