Isaiah 51:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inueni macho mzitazame mbingu, kisha tazameni dunia huko chini. Mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama vazi, na wakazi wake watakufa kama wadudu. Lakini wokovu niuletao wadumu milele; ukombozi wangu kamwe hautakoma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame dunia chini; mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama vazi, na wakazi wake kufa kama inzi. Bali wokovu wangu utadumu milele, haki yangu haitakoma kamwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inueni macho mzitazame mbingu, kisha tazameni dunia huko chini. Mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama vazi, na wakazi wake watakufa kama wadudu. Lakini wokovu niuletao wadumu milele; ukombozi wangu kamwe hautakoma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame dunia chini; mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama vazi na wakazi wake kufa kama mainzi. Bali wokovu wangu utadumu milele, haki yangu haitakoma kamwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame dunia chini; mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama vazi, na wakazi wake kufa kama mainzi. Bali wokovu wangu utadumu milele, haki yangu haitakoma kamwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na ukombozi wangu hautakoma kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inueni macho mzitazame mbingu, kisha tazameni dunia huko chini. Mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama vazi, na wakazi wake watakufa kama wadudu. Lakini wokovu niuletao wadumu milele; ukombozi wangu kamwe hautakoma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yaelekezeni macho yenu mbinguni! Kisha zitazameni nchi zilizoko chini! Kwani mbingu zitatoweka kama moshi, nazo nchi zitachakaa kama nguo, nao wazikaliao mara watakufa vivyo hivyo. Lakini wokovu wangu utakuwa wa kale na kale, nao wongofu wangu hautaangamika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muinue macho, muangalie mbingu, kisha muangalie dunia kule chini. Mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama nguo, na wakaaji wake watakufa kama vidudu. Lakini wokovu ninaouleta unadumu milele; ukombozi wangu hautakoma hata kidogo.