Isaiah 51:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amka! Amka ee Mwenyezi-Mungu! Jivike nguvu zako utuokoe. Amka kama ulivyofanya hapo zamani, nyakati za vizazi vya hapo kale. Je, si wewe uliyemkatakata Rahabu, ukalitumbua dude hilo la kutisha?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amka, Amka! Jivike nguvu, ewe mkono wa Mwenyezi Mungu, Amka, kama siku zilizopita, kama vile vizazi vya zamani. Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande, uliyemchoma huyo mnyama mkubwa?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amka! Amka ee Mwenyezi-Mungu! Jivike nguvu zako utuokoe. Amka kama ulivyofanya hapo zamani, nyakati za vizazi vya hapo kale. Je, si wewe uliyemkatakata Rahabu, ukalitumbua dude hilo la kutisha?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amka, Amka! Jivike nguvu, Ewe mkono wa BWANA, Amka, kama vile siku zilizopita, kama vile katika vizazi vya zamani. Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande, uliyemchoma yule joka?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amka, Amka! Jivike nguvu, ewe mkono wa bwana, Amka, kama siku zilizopita, kama vile vizazi vya zamani. Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande, uliyemchoma yule joka?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amka! Amka ee Mwenyezi-Mungu! Jivike nguvu zako utuokoe. Amka kama ulivyofanya hapo zamani, nyakati za vizazi vya hapo kale. Je, si wewe uliyemkatakata Rahabu, ukalitumbua dude hilo la kutisha?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amka! Amka, uone nguvu, wewe mkono wa Bwana! Amka kama siku za kale kwenye vizazi vya zamani! Si wewe uliomkatakata Rahabu (Mkuu wa maneno wa Misri) na kumchoma yule joka kubwa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amuka! Amuka na nguvu, ee mukono wa Yawe! Amuka kama ulivyofanya hapo zamani, nyakati za vizazi vilivyopita. Si wewe ndiwe uliyemukatakata yule nyama mukubwa Rahabu, ukamutoboa yule nyoka mukubwa wa kuogopesha?