Isaiah 52:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ondokeni! Ondokeni! Tokeni hapa; msiguse kitu chochote najisi! Ondokeni huku Babuloni! Jitakaseni enyi mbebao vyombo vya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ondokeni, ondokeni, tokeni huko! Msiguse kitu chochote kilicho najisi! Tokeni kati yake mwe safi, ninyi mchukuao vyombo vya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ondokeni! Ondokeni! Tokeni hapa; msiguse kitu chochote najisi! Ondokeni huku Babuloni! Jitakaseni enyi mbebao vyombo vya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ondokeni, ondokeni, tokeni huko! Msiguse kitu kilicho najisi! Tokeni kati yake mwe safi, ninyi mchukuao vyombo vya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ondokeni, ondokeni, tokeni huko! Msiguse kitu chochote kilicho najisi! Tokeni kati yake mwe safi, ninyi mchukuao vyombo vya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ondokeni! Ondokeni! Tokeni hapa; msiguse kitu chochote najisi! Ondokeni huku Babuloni! Jitakaseni enyi mbebao vyombo vya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ondokeni! Ondokeni! Tokeni hapa! Msiguse yenye uchafu! Tokeni humu kati! Jitakaseni, ninyi mnaovichukua vyombo vya Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muondoke! Muondoke! Mutoke pale! Musiguse kitu chochote kichafu! Muondoke kule Babeli! Mujitakase, enyi munaobeba vyombo vya Yawe.