Isaiah 52:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jikungute mavumbi, uinuke ewe Yerusalemu uliyetekwa nyara! Jifungue minyororo yako shingoni, ewe binti Siyoni uliyechukuliwa mateka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jikung’ute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha utawala, ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, ee Binti Sayuni uliye mateka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jikung'ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jikung'ute mavumbi, uinuke ewe Yerusalemu uliyetekwa nyara! Jifungue minyororo yako shingoni, ewe binti Siyoni uliyechukuliwa mateka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jikung'ute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, Ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako. Ee Binti Sayuni uliye mateka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jikung’ute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, ee Binti Sayuni uliye mateka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jikung'ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungue vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jikungute mavumbi, uinuke ewe Yerusalemu uliyetekwa nyara! Jifungue minyororo yako shingoni, ewe binti Siyoni uliyechukuliwa mateka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakung'ute mavumbi, kisha inuka, upate kukaa, Yerusalemu! Yafungue mafungo yaliyopo shingoni pako, binti Sioni, uliofungwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jikung’ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ujikungute mavumbi, usimame, ewe Yerusalema uliyekuwa mufungwa! Ujifungue minyororo yako katika shingo, ewe binti Sayuni uliyekamatwa mateka.