Isaiah 53:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumiza na kumweka katika huzuni. Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi. Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa; ataishi maisha marefu. Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kumchubua na kumsababisha ateseke. Ingawa Mwenyezi Mungu amefanya maisha yake kuwa sadaka ya hatia, ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, nayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu yatafanikiwa mkononi mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumiza na kumweka katika huzuni. Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi. Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa; ataishi maisha marefu. Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yalikuwa ni mapenzi ya BWANA kumchubua na kumsababisha ateseke, ingawa BWANA amefanya maisha yake kuwa sadaka ya hatia, ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, nayo mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yalikuwa ni mapenzi ya bwana kumchubua na kumsababisha ateseke. Ingawa bwana amefanya maisha yake kuwa sadaka ya hatia, ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, nayo mapenzi ya bwana yatafanikiwa mkononi mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumiza na kumweka katika huzuni. Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi. Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa; ataishi maisha marefu. Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana alipendezwa na kumwumiza, asipone, kwamba: Atakapojitoa kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi kwa ajili ya makosa ya watu, ndipo, atakapopata mazao, ndipo, siku zake zitakapoanzia kuwa nyingi, nayo yampendezayo Bwana yatatimizwa na mkono wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe alipenda kumuponda kwa mateso. Alitoa uzima wake kwa ajili ya kuondoa zambi. Mutumishi wa Mungu atakuwa na wazao; ataishi maisha marefu. Yeye ndiye atakayetimiza mupango wa Yawe.