Isaiah 53:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, nitamweka katika cheo cha wakuu, atagawa nyara pamoja na wenye nguvu; kwa kuwa alijitolea mwenyewe kufa, akawekwa katika kundi moja na wakosefu, alizibeba dhambi za watu wengi, akawaombea msamaha hao wakosefu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, na kuwaombea wakosaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, nitamweka katika cheo cha wakuu, atagawa nyara pamoja na wenye nguvu; kwa kuwa alijitolea mwenyewe kufa, akawekwa katika kundi moja na wakosefu, alizibeba dhambi za watu wengi, akawaombea msamaha hao wakosefu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, na kuwaombea wakosaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, na kuwaombea wakosaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, nitamweka katika cheo cha wakuu, atagawa nyara pamoja na wenye nguvu; kwa kuwa alijitolea mwenyewe kufa, akawekwa katika kundi moja na wakosefu, alizibeba dhambi za watu wengi, akawaombea msamaha hao wakosefu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nitamgawia wengi, wawe fungu lake, naye atawagawia wanguvu mateka yao, yawe mafungu yao, kwa kuwa ameimwaga roho yake, ife, akahesabiwa kuwa mwenzao wapotovu. Naye ameyachukua makosa ya watu wengi, akawaombea nao wapotovu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo nitamugawanyia sehemu pamoja na wakubwa, atagawanya vitu vilivyotekwa pamoja na wenye nguvu. Alijitoa yeye mwenyewe hata kufa; aliwekwa kundi moja na watu wakosaji. Alizibeba zambi za watu wengi, akawaombea musamaha hao wakosaji.