Isaiah 53:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu, mtumishi wake alikua kama mti mchanga, kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza, wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake, hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu, mtumishi wake alikua kama mti mchanga, kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza, wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvuta kwake, hakuwa na cho chote katika kuonekana kwake cha kutufanya tumtamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake, hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu, mtumishi wake alikua kama mti mchanga, kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza, wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alikua machoni pake kama mche, kama chipuko la shina lililoko katika nchi kavu, hakuwa mwenye uzuri wala mwenye utukufu wa mwili, tulipomtazama, hakuna umbo lililotupendeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, mbele ya Yawe, mutumishi wake alikomaa kama kichipukizi, kama muzizi katika inchi kavu. Hakukuwa na umbo wala sura ya kupendeza, wala hakukuwa na uzuri wowote wa kutuvuta.