Isaiah 53:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa; na hakuna mtu aliyejali yanayompata. Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai, kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa; na hakuna mtu aliyejali yanayompata. Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai, kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kukamatwa na kuhukumiwa aliondolewa. Ni nani atakayeweza kueleza kuhusu kizazi chake? Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani angeyajali? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa; na hakuna mtu aliyejali yanayompata. Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai, kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ameuawa kwa kusongwa na kwa kunyimwa uamuzi mnyofu, lakini kwao wa kizazi chake yuko nani ayawazaye kwamba: Ameondolewa katika nchi yao walio hai, alipopigwa kwa ajili ya upotovu wao walio ukoo wake?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alikamatwa kwa kinguvu, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa; na hakuna mutu aliyejali mambo yanayomupata. Alifukuzwa kutoka inchi ya wanaokuwa wazima, kwa sababu ya makosa ya watu wangu.