Isaiah 54:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Imba kwa shangwe ewe uliye tasa, wewe ambaye hujapata kuzaa! Paza sauti na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kujifungua mtoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Imba, ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, wewe ambaye kamwe hukupata uchungu; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Imba kwa shangwe ewe uliye tasa, wewe ambaye hujapata kuzaa! paza sauti na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kujifungua mtoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Imba, Ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, ninyi ambao kamwe hamkupata utungu wa kuzaa; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Imba, ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, wewe ambaye kamwe hukupata utungu; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na uchungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Imba kwa shangwe ewe uliye tasa, wewe ambaye hujapata kuzaa! Paza sauti na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kujifungua mtoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Shangilia, wewe uliye mgumba, usiyezaa! Jichekelee na kupaza sauti, wewe usiyeona uchungu wa kuzaa! Kwani wana wake yule aliye peke yake ni wengi kuliko wana wake yule aliye na mumewe; ndivyo, Bwana anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Imba kwa shangwe, ewe unayekuwa tasa, wewe ambaye haujapata kuzaa! Piga kelele na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kuzaa mutoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa yule anayekuwa na mume.