Isaiah 54:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Milima yaweza kutoweka, vilima vyaweza kuondolewa, lakini fadhili zangu hazitakuondoka, agano langu la amani halitaondolewa. Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, wala agano langu la amani halitaondolewa,” asema Mwenyezi Mungu, mwenye huruma juu yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Milima yaweza kutoweka, vilima vyaweza kuondolewa, lakini fadhili zangu hazitakuondoka, agano langu la amani halitaondolewa. Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ijapotikisika milima na vilima viondolewe, hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, wala Agano langu la amani halitaondolewa,” asema BWANA, mwenye huruma juu yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, wala agano langu la amani halitaondolewa,” asema bwana, mwenye huruma juu yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Milima yaweza kutoweka, vilima vyaweza kuondolewa, lakini fadhili zangu hazitakuondoka, agano langu la amani halitaondolewa. Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ijapo milima iondoke, ijapo navyo vilima vitikisike, upole wangu hautaondoka kwako, wala agano la utengemano wangu halitatikisika; ndivyo, Bwana akuhurumiaye anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Milima inaweza kutoweka, vilima vinaweza kuondolewa, lakini rehema zangu kwako sitaziacha, agano langu la amani litaimarishwa. Ni Yawe anayekuhurumia anayesema hivyo.