Isaiah 54:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Silaha zote zilizoundwa kukudhuru wewe hazitafaa chochote kile. Mtu akikushtaki mahakamani, utamshinda. Hilo ndilo fungu nililowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowathibitishia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa, nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushtaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa Mwenyezi Mungu na hii ndiyo haki yao inayotoka kwangu,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Silaha zote zilizoundwa kukudhuru wewe hazitafaa chochote kile. Mtu akikushtaki mahakamani, utamshinda. Hilo ndilo fungu nililowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowathibitishia.” Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa, nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushitaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa, nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushtaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa bwana na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Silaha zote zilizoundwa kukudhuru wewe hazitafaa chochote kile. Mtu akikushtaki mahakamani, utamshinda. Hilo ndilo fungu nililowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowathibitishia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna mata yatakayozimaliza kazi zao yakiwa yametengenezwa ya kukuumiza, nao kila ulimi utakaokuinukia shaurini utashinda na kuupatilizia mabaya; hilo ndilo fungu, watumishi wake Bwana watakalolitwaa, hilo ndilo pato la wongofu wao, nitakalowapatia; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Silaha zote zilizotengenezwa kwa kukuzuru wewe hazitafaa kwa kitu chochote. Mutu akikushitaki, utamushinda. Hiyo ndiyo haki niliyowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowahakikishia. –Ni ujumbe wa Yawe.